[Swahili Special] Fikra Elekezi, Uoga na Kutokuwajibika

[Swahili Special] Fikra Elekezi, Uoga na Kutokuwajibika

Tukitaja neno Ajira; kama taswira inayokuja kichwani mwako ni kuamka asubuhi; kuvaa vizuri na kwenda ofisini kule mjini —wewe una Fikra Elekezi. Uko nyuma ya muda.


Kama bado unakomaa kutafuta fursa kwenye kile ulichokisomea tu, wewe ni mhanga wa Fikra Elekezi. Umefunga akili kwenye vyeti.?


Unavyowatamani kina John Ulanga kwa kupewa teuzi na kupanda vyeo, una hatari ya kuingia kwenye fikra elekezi. Hawa wazee ni masalia ya wanufaika wa mfumo wa zamani wa kazi na ajira. Yaani, a linear career progression. Siku hizi uhalisia uko tofauti.


Wasikilize wazee kwa busara za maisha. Wapuuze wakikupa career advice. Watakupoteza!


Uoga ni janga la kitaifa

Mwalimu Nyerere hakuwa muoga. Hakuwa na fikra elekezi. Alisimamia mawazo yake. Kwenye shinikizo la kubinafsisha, Nyerere alikataa. Alidai kwamba huwezi kuweka bondia wa uzito wa juu na mwingine kimbaumbau kwenye ulingo wapigane. Umeshaona Benki ya NBC ina tawi kule New York?


Hizi sifa za ujasiri na msimamo ni adimu mno kwa sisi vijana wa siku hizi. Uoga, kujipendekeza na uchawa ndiyo sifa kuu za kijana wa Kitanzania. Tunataka kupendwa, kukubaliwa na kupongezwa kwa gharama yoyote ile.?


Kama alivyo sema Mwalimu, wengine tunanunuliwa kama malaya. We are “mercenaries!”


Kutokuwajibika

Tatizo kubwa la vijana Tanzania ni kwamba tunazipigia makofi mamlaka zaidi kuliko kutazama na kukosoa utendaji wake. You are not supposed to clap for the hierarchy. You are supposed to WATCH it. Ni wajibu wetu vijana kuweka bayaka upuuzi wa kimfumo, sera na utendaji kwenye jamii. Siyo kuwafanya watawala ma-celebrities.


Kama kuna upuuzi wa kisera na mfumo unauona, na unashindwa kusema huu ni upuuzi --wewe ni mwoga and a f*king fraud.


Narudia tena, hutakiwi kumsifia mwanasiasa wala boss wako. Imeshadhirihika mara nyingi kwamba hawa viumbe huegemea mlengo wa rushwa na ubabe ukiwasifia sana.


Watch the hierarchy. Because they tend to tilt towards tyranny.


Naomba nikuache na hili la kufatakari

Habari za watu walio tofauti husambaa haraka kama moto wa msituni. Majina ya watu hawa, kama lilivyo jina Julius Kambarage Nyerere, hudumu vizazi hadi vizazi. Hivyo, kama haujulikani kuanzia ngazi ya mtaa, wilaya, mkoa hadi ngazi ya digitali, kuna uwezekano wewe ni muhanaga wa Fikra Elekezi.


Asante kwa kusoma.



Makala kwenye chapisho hili liitwalo Social Rhetoric huwa zinahusu uwasilishaji wenye ufanisi. Huwa ninaandika kwa Kiingereza. Leo nimeona niandike kwa Kiswahili ili kumuenzi Mwl. Julius Nyerere –Baba wa Taifa langu, Tanzania.



Alex Shayo

Working with Team Leaders to avoid falling short of their targets by keeping their teams continually accountable, ensuring continuous profitable growth.

1 年

Thoroughly enjoyed reading this one.

回复
ALLY MSANGI

Content Marketer and SEO Guy | Building digital products and online businesses and sharing the process with others.

1 年

Umendika kwa hasira na uchungu sana kusema ukweli. Vijana tumezidi kuwa tegemezi wa fikra. Tuna kizazi cha uchawa na sio kizazi kinacho enzi watu mahiri na shupavu wenye misimamo kama Nyerere. Kujipendekeza na uchawa ndio kumetawala vijana leo hii. Vijana sasa wana waza kuajiriwa zaidi kuliko kujifungulia fursa kwenye ulimwengu huu wa Digitali. Tuamke aisee.

回复

Njaaaa mbaya, imeua vijana wanamapinduzi wa fikra, tumebakiwa na CHAWA.

Eunice Lyimo

Marketing Communication Strategist|Media Planning|Project management|Leadership|Business Development

1 年

Shukuru nakukubali sana kaka..Fikra elekezi zinashusha confidence vibaya sana.

回复
Godlove Festo

Digital Marketing Strategist | Writer & Brand Growth Expert.

1 年

Hahaha nime enjoy the reading "Kama alivyo sema Mwalimu, wengine tunanunuliwa kama malaya." kipande hiki nimekisoma kwa sauti ya ile speech yake.

要查看或添加评论,请登录

Shukuru Amos的更多文章