Mafua Yasiyoisha Kwa Watoto
Ibrahim Msangi
Medical Doctor Dedicated to Providing Evidence-Based Information to Enhance Health | General Practice | Health Writer | Men Health | Digital Health
?Mafua yasiyoisha kwa Watoto
Ninapokuwa clinic wazazi wengi huja na Watoto wao wakiwa wanasumbuliwa na mafua.
Mara nyingi mafua haya huwasumbua Watoto mara kwa mara na wazazi wengi huwa na shauku ya kuona Watoto wao hawateseki na hali hii wanapokuja clinic.
Ila ni ngumu kwa mtoto kutokupata maradhi haya.
Hii ni kwa sababu watoto hawana kinga ya mwili ya kutosha kupambana na vijidudu vya mafua kama ilivyo kwa watu wakubwa. Watoto kuchanganyika pamoja katika shule na mabadiliko ya hali ya hewa pia huchangia mafua ya mara kwa mara.
Tafiti zinaonyesha kuwa kwa mafua, ugonjwa unaeza kuchukua muda wa wiki 2 kupona wenyewe bila kutumia dawa. Pia mafua mara nyingi husababishwa na virusi na sio bakteria. Hivyo dawa za antibiotic hazina manufaa katika matibabu.
Mara nyingi wazazi huhisi antibiotic ni suluhisho la mafua kwa watoto wao, hivyo baadhi huja wakiwa tayari wameshawapa antibiotic Watoto bila mafanikio. Jambo hili ni hatari maana huweza kusababisha usugu wa dawa na kushindwa kutibu mara zinapohitajika kweli.
Muhimu kwa wazazi kufahamu ni kuwa mara nyingi mafua unaweza kuyatibu nyumbani kwa kutibu dalili Zaidi mfano kama mtoto ana homa basi kutumia parecatamol na kuongeza maji na vimiminika zaidi. Inabidi kwenda hospitali endapo:
·????????Kukataa kula au kunywa kwa muda mrefu
·????????Kuchoka sana
·????????Kupata shida kupumua
·????????Homa isiyoshuka hata baada ya kutumia paracetamol
·????????Kutapika sana
·????????Dalili za maambukizi ya masikio kama vile kuvuta sikio, au sikio kuuma au kutoa majimaji au usaha
Iwapo dalili hizo za hatari hazijaonekana basi siyo lazima kuwa na hofu kwani mafua ya aina hiyo huisha yenyewe bila madhara yoyote.
Tukiongelea kuhusu kinga basi ni muhimu kwa wazazi kuwafundisha watoto wao yafuatayo ili kupunguza mafua ya mara kwa mara:
·????????Kuwafundisha Watoto kunawa mikono vizuri pindi wanapoenda msalani na wanapotoa mafua au kugusa pua. Hii huzuia maambukizi kujirudia rudia au kuhamia sehemu nyingine za mwili kama macho.
·????????Kuzuia mdomo pale wanapokohoa au kupiga chafya. Hii inazuia kuendeleza maambukizi kwa wengine.
·????????Kula mbogamboga na matunda kwa wingi kwani vyakula hivi vina vitamini na madini yanayochochea kinga zao za mwili.
·????????Kunywa maji safi ya kutosha.
·????????Kuhakikisha Watoto wanapata muda wa kutosha wa kulala ili kukua vyema na kuimarisha kinga zao za mwili.