JINSI YA KUANZISHA BIASHARA 
YA SPARE ZA MAGARI

JINSI YA KUANZISHA BIASHARA YA SPARE ZA MAGARI

1. INTRODUCTION

Jinsi ya kuanzisha biashara ya spare za magari ni muendelezo wa video zetu zinatolewa kwenye program ya Good Morning Tanzania https://youtu.be/EtR9DOIdLkI

Kati ya biashara zenye mvuto Tanzania miaka ya karibuni, moja wapo ni ile ya spare za magari

Kuna wajasiriamali wengi ambao wanamiliki maduka ya spare za magari hapa Tanzania. Wengine wanafanya biashara nzuri na kuna wengine biashara zao haziko vizuri.

Kama wewe unataka kuanzisha biashara ya spare za magari basi nisikilize kwa makini ili na wewe uwe na biashara ambayo iko vizuri.

Siri ya mafanikio ya biashara ya spare za magari ni ipi?

Siri ya mafanikio ya biashara ya spare za magari ni pale mjasiriamali anapo tekeleza taratibu zinazo kubalika za kuanzisha na kuendeleza hiyo biashara

Kama nilivyokwisha kueleza kwenye video zangu zililizopita, usianzishe biashara ya spare za magari mpaka pale utakapoona kuna fursa ya kufanya hiyo biashara

Nimekuwa nikisema kuwa siku zote fursa ya kufanya biashara hujitokeza kwa kuangalia changamoto za wateja

2. CHANGAMOTO ZA WATEJA

Jambo la msingi ni kuangalia changamoto mbali mbali zinazo wakabili wateja wa spares za magari na kuzigeuza kuwa fursa ya kufanya biashara

Sasa basi zipi ni changamoto za wateja wa spare za magari?

Kuna changamoto nyingi zinazo wakabili wateja wa spare za magari.

Baadhi ya hizo changamoto ni kama zifuatazo:

(a)????Eneo linalohusika hakuna kabisa maduka ya spare za magari

(b)????Eneo linalohusika hakuna maduka yenye spares ya baadhi ya magari

(c)?????Eneo linalohusika kuna maduka yanayo uza spare za magari za ubora mdogo

(d)????Eneo linalo husika maduka ya spare bei zake ziko juu sana

Jambo la msingi ni kuhakikisha una anzisha duka la spare ambalo litakuwa na ufumbuzi wa baadhi ya changamoto zinazo wakabili wateja

?3. MAMBO MUHIMU 11 WAKATI WA KUANZISHA?BIASHARA YA SPARE ZA MAGARI

Mambo 11 ambayo itabidi utekeleze ni kama ifuatavyo:

?3.1???Chagua aina ya wateja kuhudumia

Fanya uamuzi wa aina ya wateja utakao wahudumia kutegemea aina ya spare za magari unazotaka kuuza

3.2 Chagua mahali pa duka la spare

Weka duka la spare kwenye barabara kubwa na zenye magari mengi au sehemu yenye mkusanyiko mkubwa wa magari. Mfano ni karibu na stendi ya mabasi, kitua cha daladala au kwenye garage za magari

3.3 Uchaguzi wa spares zenye mvuto kwa wateja

Fahamu aina spares zenye mvuto kwa wateja wengi. Hii inategemea model ya magari na aina ya gari kama ni gari ndogo, kubwa, mabasi, malori nk

3.4???Fahamu vifaa vya duka la spares

Fahamu vifaa vinavyo hitajika kwa ajiri ya duka la spares.Mifano ni kama vile mizani, computer, makasha ya kuweka spares, frame za kupanga spares nk

3.5???Upangaji wa bei za spares

Panga bei zenye mvuto kwa wateja. Zisiwe za juu hivyo kufukuza wateja au za chini ambazo zitasababisha upate hasara

3.6???Ununuzi wa spare za magari

Kama una mataji mkubwa wa biashara ni vizuri kuagiza spares za magari kutoka nje ya nchi ili upate spare bora na kwa bei nafuu.

Kama mtaji mdogo nunua spares kutoka kwenye maduka makubwa ya spares

3.7 Uza bidhaa zingine zinazo husiana na spares

Hakikisha duka lako la spare pia linatoa huduma za bidhaa nyingine kama mapambo, radio nk

3.8 Tengeneza budget ya duka la spares

Tengeneza bajeti inayo kidhi matakwa ya biashara ya spares za magari

3.9 Mtaji wa biashara ya spares za magari

Fahamu jinsi utakavyopata mtaji wa biashara yako ya matunda. Angalia video zangu kuhusu jinsi ya kufanya makisio ya mtaji wa biashara kwenye You Tube channel ya Ali Mwambola

3.10 Tangaza biashara ya duka la spares

Weka mabango yanayotangaza duka la spares. Pia tangaza biashara kutumia mitandao ya jamii. Unaweza kutumia mitandao ya kijamii kama facebook, Instagram na Twitter. Wateja wanaweza kuweka order zao za spares kupitia mitandaoni

3.11 Weka hesabu za biashara yako????????????

Ni vizuri kuweka utaratibu wa kuweka hesabu za biashara yako ya matunda ili ufahamu kama unapata faida au hasara

Kuangalia video bonyeza link inayofuata https://youtu.be/EtR9DOIdLkI

uchambuzi mridhawa huu

回复
Michael Falato

GTM Expert! Founder/CEO Full Throttle Falato Leads - 25 years of Enterprise Sales Experience - Lead Generation and Recruiting Automation, US Air Force Veteran, Brazilian Jiu Jitsu Black Belt, Muay Thai, Saxophonist

1 个月

Ali, thanks for sharing! I am hosting a live monthly roundtable every first Wednesday at 11am EST to trade tips and tricks on how to build effective revenue strategies. I would love to have you be one of my special guests! We will review topics such as: -LinkedIn Automation: Using Groups and Events as anchors -Email Automation: How to safely send thousands of emails and what the new Google and Yahoo mail limitations mean -How to use thought leadership and MasterMind events to drive top-of-funnel -Content Creation: What drives meetings to be booked, how to use ChatGPT and Gemini effectively Please join us by using this link to register: https://forms.gle/iDmeyWKyLn5iTyti8

回复
Matt Knueven

Sales Manager @ One Direct Health Network | Business Development, Medical Device Sales

4 个月

Ali, thanks for sharing!

回复

要查看或添加评论,请登录