Tanzania Forest Service Agency/ Wakala wa Huduma za Misitu (TFS)
林业和木业
Sustainably managing national forests and bee resources
关于我们
We aim to sustainably manage national forests and bee resources in order to contribute to the social, economic, ecological and cultural needs of present and future generations
- 网站
-
https://www.tfs.go.tz
Tanzania Forest Service Agency/ Wakala wa Huduma za Misitu (TFS)的外部链接
- 所属行业
- 林业和木业
- 规模
- 超过 10,001 人
- 类型
- 政府机构
Tanzania Forest Service Agency/ Wakala wa Huduma za Misitu (TFS)员工
动态
-
NYUKI MARATHON A BIG SUCCESS The Nyuki Marathon in Arusha marked an important milestone as participants and organizers prepared for the upcoming Apimondia Congress in 2027. With over 500 runners from various countries, the event celebrated athleticism while highlighting the crucial role of beekeeping in environmental conservation. During the marathon, David Mukomana, President of the Apimondia Regional Commission for Africa, emphasized the importance of bees as essential pollinators and contributors to sustainable development. "This event is special to me personally and crucial for Tanzania as we approach the 2027 Congress," Mukomana stated. Arusha's Mayor, Maximilian Iranghe, announced a plan to distribute 2 million beehives to boost the local bee population, saying, "We want Arusha to have many bees; the Apimondia Congress will be a catalyst for development." Restetuta Lopes Lazarus, Executive Director of Worker Bees Africa, noted that the marathon aimed to raise awareness about the importance of bees for human life and highlight honey's medicinal properties for various ailments. Professor Dos Santos Silayo, Commissioner of the Tanzania Forest Service (TFS), urged citizens and stakeholders in beekeeping to seize the opportunities presented by the upcoming global beekeeping congress. He emphasized that beekeeping is a business and supports tourism and conservation efforts. Speaking at the Nyuki Marathon on October 26, 2024, Prof. Silayo remarked that this was the first marathon of its kind in the world, crucial for the growth of the beekeeping sector both nationally and internationally. "As we prepare for the 50th Apimondia Congress in 2027, this event sends a strong message that Tanzania is ready," he stated. Prof. Silayo underscored that effective environmental management is key to bee production, which in turn boosts local economies. "Bees are an asset; they must be nurtured with proper beehives, and the environment must be protected," he concluded. The Nyuki Marathon not only celebrated athletic achievement but also served as a vibrant reminder of the collective efforts needed to champion beekeeping and protect our planet, paving the way for a sustainable future leading up to Apimondia 2027. #apimondia2027 #apimondia #bees #honey
-
+6
-
???????????????? ?????????????????? ?????? ?????????????? ???? ?????????? ???? ?????????????? ?????????? 2027 ---???????????? ???????????????????????? ?????????????? ?????????? ???????????????? ???????????? KAMISHNA wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo, amewataka wananchi na wadau wa ufugaji nyuki nchini kuchangamkia fursa ya Mkutano wa Dunia wa Ufugaji wa Nyuki (Apimondia) utakaofanyika mwaka 2027. Akizungumza katika Nyuki Marathon iliyofanyika leo Oktoba 26,2024 Jijini Arusha, Prof. Silayo alisisitiza kwamba ufugaji nyuki si tu ni biashara bali pia unachangia katika ukuzaji wa utalii na uhif-dhi. Marathoni hiyo ilihusisha wanariadha takriban 500 kutoka mataifa mbalimbali, ikiwa na lengo la kuhamasisha ufugaji wa nyuki na kutangaza umuhimu wa mazingira. Prof. Dos Santos alisisitiza kuwa mashindano hayo ya Nyuki marathon ni ya kwanza duniani na mashindano muhimu kwa afya, ukuwaji wa sekta ya nyuki nchini na duniani sambamba na kujenga mahusiano mema ya nchi yetu kimataifa kwa sababu yameleta watu wa mataifa mbalimbali kuja kushiliki mashindano hayo. "Lakini kwakuwa tunajiandaa kama sehemu ya kufanyika kwa Kongress ya 50 ya Apimindia 2027 hapa nchini imekuwa sehenu nzuri sana yakutuma ujumbe kwamba Tanzania tuko tayari, " anasema. Anaongeza kuwa utunzaji mzuri wa mazingira unachangia katika uzalishaji wa nyuki, na hivyo kuongeza uchumi wa jamii. "Nyuki ni mtaji; wanapaswa kutunzwa kwa kutumia mizinga na mazingira lazima yalindwe," alisema. David Mukomana, Rais wa Kamati ya Kanda ya Apimondia kwa Afrika, alisisitiza umuhimu wa tukio hili kama jukwaa la kuhamasisha ufahamu kuhusu ufugaji nyuki. Alieleza, "Nyuki Marathon ni hatua muhimu kuelekea mwaka 2027. Tunaweza kujenga ustahimilivu wa jamii kupitia ufugaji nyuki." Mukomana alieleza uhusiano wake wa kibinafsi na tukio hili, akisema, "Nyuki Marathon ni jambo la pekee sana kwangu. Linawakilisha hatua muhimu kuelekea mwaka 2027, natambua uwepo wa Meya wa Arusha kama ishara ya kuonyesha utayali wa jiji hili na Tanzania kuelekea kongamano lijalo." Meya wa Jiji la Arusha, Maximilian Iranghe, alitangaza mpango wa kugawa mizinga milioni 2, akisisitiza lengo la kuongeza idadi ya nyuki katika eneo hilo. "Tunataka Arusha iwe na nyuki wengi; mkutano wa Apimondia utakuwa chachu katika kuleta maendeleo," alisema. Wakati huo huo, Restetuta Lopes Lazarus, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Woker Bees Africa, aliongeza kwamba mbio hizo zililenga kuelezea umuhimu wa nyuki kwa maisha ya binadamu, akisisitiza kwamba asali ni tiba kwa magonjwa mbalimbali. Marathoni hiyo, iliyopewa kauli mbiu "Kuelekea Apimondia 2027," ilidhihirisha umuhimu wa ushirikiano wa ndani na wa kimataifa katika kukuza ufugaji wa nyuki na kulinda mazingira.
-
+3
-
*TFS Yapongezwa na Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC)* *Dodoma, 15 Oktoba 2024* Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imeipongeza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa mafanikio yake katika kutekeleza majukumu yake. Pongezi hizo zilitolewa na Mwenyekiti wa kamati, Mhe. Augustine Vumma Hole, wakati wa semina iliyofanyika leo kwa ajili ya kuwasilisha mkakati wa TFS katika kuongeza mapato ya Serikali na kuimarisha uhifadhi. "Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayofanya, ambapo mmekuwa na mchango wa bilioni 25 kwenye mfuko mkuu wa Serikali kwa mwaka wa fedha 2023/24," alisema Mhe. Hole. Meneja Mipango wa TFS, Bi. Neema Mbise, alieleza kwamba mapato ya TFS yameendelea kukua, yakifikia bilioni 165.58 kwa mwaka huu. Aliongeza kuwa, "uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali na dhamira ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ndiyo sababu kuu ya ukuaji huu na uhifadhi kuimarika." Kamishna wa Uhifadhi TFS, Prof. Dos Santos Silayo, alipokea pongezi hizo na kutoa ufafanuzi kuhusu hoja mbalimbali za wajumbe wa kamati. Prof. Silayo pia alizungumza kuhusu mikakati mbalimbali ya TFS, ikiwemo biashara ya kaboni ambayo inatarajiwa kuleta Dola milioni 65.4 kwa mwaka, kuongeza mapato kupitia utalii wa ikolojia, na kukuza uzalishaji wa mazao ya misitu na nyuki. "Katika kipindi cha miaka minne, Wakala umeweza kukusanya shilingi bilioni 13.1 kutokana na biashara ya utomvu kutoka mashamba ya miti ya Sao Hill, Buhindi, na Rubya," alisisitiza Prof. Silayo. Kwa kumalizia, alieleza kuwa TFS itaendelea na usimamizi madhubuti na matumizi endelevu ya rasilimali za misitu na nyuki, kuhakikisha kwamba maendeleo yanafikiwa bila kuathiri mazingira.
-
+3
-
*TFS Yaibuka na Utalii wa Nyuki Katika Maonesho ya SITE 2024* Dar es Salaam, Oktoba 11, 2024 – Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) leo imekuwa kivutio kikubwa katika Maonesho ya Nane ya Kimataifa ya Swahili International Tourism Expo (SITE), yaliyofunguliwa rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam. TFS, moja ya washiriki wakuu, imepata nafasi ya kuonyesha fursa za kipekee za utalii ikolojia nchini, huku ikiibua vivutio vipya ambavyo vimewafanya watu kushiriki kwa hamasa kubwa. Katika banda lake, TFS inawasilisha fursa za uwekezaji kwenye maeneo inayaoyasimamia kama vile maeneo ya kihistoria ya Magofu ya Tongoni Ruins, Kaole Ruins, na Mji Mkongwe wa Bagamoyo, pamoja na vivutio vya utalii wa kiikolojia vilivyoko kwenye hifadhi zake. Hata hivyo, kilichovuta hisia zaidi mwaka huu ni utalii mpya wa nyuki (Api-tourism), unaowapa wageni nafasi ya kipekee kudungwa na nyuki kwa lengo la tiba na kujipatia bidhaa mbalimbali zinazotokana na nyuki. Brenda Mwakipesile, mmoja wa wahifadhi kutoka TFS anayehusika na kudungisha nyuki wageni, alisema, “Utalii huu wa nyuki unazidi kuvutia watu kwa sababu ya faida zake kiafya. Nyuki wana uwezo wa kuimarisha kinga ya mwili na kusaidia kutibu maradhi mbalimbali. Wananchi wengi wanaendelea kujitokeza kupata huduma hii, na tumekuwa tukiendelea kuitoa hata baada ya maonesho katika Msitu wa Hifadhi wa Mazingira Asilia Vikindu uliopo Mkurnga mkoani Pwani.” Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Dk. Ramadhan Dau, ambaye pia alijitokeza kudungwa na nyuki katika mikono yote miwili, aliwahamasisha wananchi zaidi kufika kujionea na kushiriki katika utalii huu wa kipekee. Alisisitiza kuwa hii ni nafasi adimu ambayo si tu inasaidia afya bali pia inatoa fursa ya pekee ya kujifunza kuhusu maajabu ya nyuki. Kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, TFS imejikita kuleta aina mpya za utalii ambazo hazipatikani sehemu nyingine, huku ikihakikisha kuwa watalii wanapata uzoefu wa kipekee unaohusisha si tu vivutio vya asili bali pia tiba asilia kupitia utalii wa nyuki. Maonesho ya SITE yanaendelea hadi mwisho wa wiki, na TFS inaendelea kuwakaribisha wadau wote kufika kwenye banda lake ili kujifunza, kushiriki, na kupata huduma za kipekee zinazotolewa, ikiwemo utalii huu wa nyuki unaovutia watu wa rika zote.
-
+2